Seminari yafanya hija kwenda Nairobi

Katika wiki in albis ya mwaka 2018 (inayofuata Pasaka), walezi na waseminari walifanya hija kwenda Nairobi. Pale walitembelea Ubalozi wa Baba Mtakatifu nchini Kenya, na majimbo ya Nairobi na Ngong. Pia waliadhimisha Ekaristi kwenye parokia mbalimbali za jiji, na walipata fursa ya kucheza mchezo wa kirafiki pamoja na vijana wa Jumuiya za Neokatekumenato za Nairobi.