Seminari ya aina mpya kwa Uinjilishaji Mpya
Seminary yetu ni moja kati ya Seminari Redemptoris Mater zaidi ya 120 ulimwenguni kote. Seminari hizi ni tunda la upyaisho ulioletwa na Mtaguso wa Vatikano II, uliovuvia msukumo mpya wa kimisionari katika Kanisa Katoliki lote. Pia ni tunda la Njia ya Neokatekumenato, ambayo ni njia ya malezi ya Kikristo ambayo sisi sote, walezi na waseminari, tunashiriki katika parokia zetu, na katika hiyo tumetambua miito yetu.
Kwa kuwa Njia ya Neokatekumenato inapendekeza upyaisho ya parokia, ni dhahiri kwamba Seminari zilizotoka Njia hii ziwe Seminari za Jimbo, lakini vile vile zenye roho ya Kimisionari na ya kimataifa, kama Roho Mtakatifu alivyovuvia karama hii ya Kanisa.
«Para organizar una solidaridad pastoral de conjunto en África, es necesario promover la renovación de la formación de los sacerdotes. Nunca se meditarán bastante las palabras del Concilio Vaticano II al afirmar que «el don espiritual que recibieron los presbíteros en la ordenación los prepara no para una misión limitada y reducida, sino para una misión amplísima y universal de salvación “hasta los confines de la tierra” (Hch 1, 8)».
«Por este motivo yo mismo exhorté a los sacerdotes a «estar concretamente disponibles al Espíritu Santo y al Obispo, para ser enviados a predicar el Evangelio más allá de los confines del propio país. Esto exigirá en ellos no sólo madurez en la vocación, sino también una capacidad no común de desprendimiento de la propia patria, grupo étnico y familia, y una particular idoneidad para insertarse en otras culturas, con inteligencia y respeto».
Yohane Paulo wa II Ecclesia in Africa, 133.
Seminari Redemptoris Mater ya Dar es Salaam [iliwekwa rasmi] mwaka 2007 na Askofu Mkuu Polycarp Kad. Pengo kwa ajili ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Toka hapo, waseminari kutoka mataifa na tamaduni mbalimbali wanapata malezi kuelekea Upadre, na 7 kati yao wameisha maliza malezi yao na wanatumikia Kanisa mahalia.
Walezi
-
Gombera
P. Michele Tronchin
Jimbo la Roma -
Gombera Msaidizi
P. Marek Saran
Jimbo la Roma
Waseminari
Sasa hivi viajana 27 kutoka mataifa 12 tofauti wanajiandaa kuelekea Upresbiteri kwenye Seminari yetu. Wote wametambua mwito wao ndani ya jumuiya ya Neokatekumenato, ambayo ni mchakato wa malezi ya Kikristo iliyotambulika na Mt. Yohane Paulo wa II kama “njia ya malezi ya Kikatoliki, inayofaa jamii na nyakati za siku hizi”:
4 wanamalizia masomo
3 katika utume kama makatekista wasafiri
1 katika utume wa kichungaji parokiani
Mapadre
-
Pd. Asis Mendoça
Asili: India
Alipadirishwa: 2007
Utume: Paroko Jimbo Kuu la DSM -
Pd. José Girón Anguiozar
Asili: Hispania
Alipadirishwa: 2016
Utume: Masomo ya shahada ya uzamili ya Theolojia -
Pd. Eduardo Santos Ramos
Asili: El Salvador
Alipadirishwa: 2017
Utume: Paroko Msaidizi Jimbo Kuu la DSM
Mashemasi
-
Alset Oyubo
Asili: Kenya
Alipata Ushemasi: 2019 -
Gregory Kijanga
Asili: Tanzania
Alipata Ushemasi: 2019 -
Murivan Brandão
Asili: Brasil
Alipata Ushemasi: 2019 -
Jaime Paim
Asili: Angola
Alipata Ushemasi: 2019